Peter Msechu apania kupunguza ‘utipwatipwa’
Peter Msechu amesema amedhamiria kuanza kufanya diet ili kupunguza mwili wake.
Msechu amesema hajalazimishwa na mtu kufanya diet, ni uamuzi wake.
“Kimsingi mimi sina tatizo, niko fit na nafanya mazoezi sana ndio maana nina uwezo wa kufanya performance hata ya live na bendi hata kwa masaa 8 bila kukaa,” amesema.
“Kwahiyo kimsingi kuamua kufanya diet ni program yangu ambayo niliamua kuifanya toka zamani sema tu nilikuwa na mambo mengi na unatakiwa ujicommit kwa kiasi fulani. Kwahiyo ni kitu ambayo nilikiplan muda mrefu nikaamua mimi mwenyewe hakuna mtu aliyenishurutisha.”
“Msechu kaamua mwenyewe hajalazimishwa, ni uamuzi wangu katika kujiweka fit,” Msechu aliiambia Story Tatu ya Planet Bongo kupitia East Africa Radio
Post a Comment