Wema Sepetu amlilia Kanumba kwenye hili
Wema Sepetu amedai hakuna msanii aliyejaribu kuendeleza juhudi za marehemu Steven Kanumba ili kuipeleka tasnia ya filamu kimataifa.
Wema ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa wapo waliojaribu lakini bado wanahitaji kuungwa mkono.
“Hilo limekwamia hapo na sifahamu kama tutaweza kujikongoja tena, wapo tunaojaribu lakini bado tunahitaji kuungwa mkono sana kuhakikisha tunafanya kama alivyofanya yeye,” alisema Wema.
“Kuigiza suala moja na kupeleka tasnia mbele suala lingine, Kanumba alimudu vyote, alifanya vizuri ndani na alijipambanua Kimataifa na kufanya sanaa ya filamu bongo itambulike nje ya Bongo,” aliongeza.
Pia Wema alieleza kwanini wasanii wengi wa filamu wanashindwa kwenda kimataifa.
“Ushindani hauridhishi, hakuna umoja wa kweli, mmeguko unaweza kuwa chanzo cha hayo, Inshallah tukijipanga tunaweza kujikwamua ingawa tunahitaji kutumia nguvu nyingi kwa sababu tumekubali kurudi nyuma,” alisisitiza.
Post a Comment