Madee: Tazama mjengo wangu huu ukupe hasira (Picha)
Madee amesema aliamua kuonesha mjengo wake baada kukamilika kwa madhumuni ya kuwatia hasira vijana wenzake wanaochezea pesa.
Madee amesema kuwa licha ya kuonesha picha ya mjengo huo, bado ana nyumba nyingine iliyopo katika hatua za mwisho.
“Hii nyumba ipo Mbezi na tayari nimeshahamia,” alisema. “Hii ni ya kwanza bado kuna moja naimalizia. Nawaonyesha makusudi ili kuwatia hasira kwa sababu vijana wanachezea pesa bila kuwekeza au kujua kuna kesho.”
Katika hatua nyingine Madee amewataka mashabiki kusubiria kazi nzuri kutoka kwake zitakazoanza kutoka hivi karibuni.
Post a Comment