Harmonize afunguka "Sijamvisha mtu pete"
Msanii
kutoka katika label WCB Wasafi Harmonize ambaye kwa sasa anafanya poa
na wimbo wake mpya wa 'Bado' amefunguka na kusema kuwa katika maisha
yake ya hajawahi kuvalishwa pete ya uchumba na wala yeye hajawahi
kumvalisha
Harmonizer akiwa na Jackline Wolper.
mtu
pete ya uchumba na kudai mpenzi wake mpya Jackline Wolper amemkuta
akiwa hana mtu na ndiyo maana wakaweza kuanzisha mahusiano.
Harmonize amesema hayo kupitia kipindi cha Enews ambapo alikuwa anaelezea mambo mbalimbali kuhusu maisha yake mapya katika mahusiano na Wolper ambaye yeye mwenyewe amekiri kuwa ni mtu aliyeanzisha naye mahusiano hivi karibuni na kusema tuwe na subira kila kitu kitakuja kuwekwa wazi siku za usoni.
"Unajua mpaka saizi sijamvisha mtu pete ya uchumba wala mimi sijawahi kuvishwa pete ya uchumba ila niseme tu ni kweli nipo kwenye mahusiano na Wolper ambaye ni maarufu kama mimi na wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi" alisema Harmonize

Post a Comment