Rungwe aonyesha wasiwasi wake na bajeti ya nchi.
Wakili
na Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Hashim Rungwe amesema kuwa bajeti
iliyopitishwa na serikali haitaweza kubadilisha maisha ya watanzania
endapo serikali haitaweka nia ya dhati ya kubana matumizi yake.
Wakili na Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Hashim Rungwe amesema kuwa bajeti iliyopitishwa na serikali haitaweza kubadilisha maisha ya watanzania endapo serikali haitaweka nia ya dhati ya kubana matumizi yake.
Akiongea na East Africa Radio ofisini kwake Bw Rungwe amesema kuwa matumizi makubwa ya serikali yanawabebesha mizigo mikubwa wananchi wa kawaida na matumizi hayo yanaonekana zaidi kwenye uwepo wa wafanyakazi wengi serikalini ambao hawana tija kwa taifa na majukumu yao yangeweza kufanywa na watendaji wengine hali inayoongeza gharama kubwa za kulipa mishahara.
Aidha Bw Rungwe ameunga mkono uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi kwani mahakama hiyo inaweza punguza vitendo vya ubadhilifu wa fedha na rushwa ambazo zinaonekana kushika kasi nchini Tanzania.
Aidha ameonya kauli ya watumishi wa umma kusema kuwa wanawasaidia wananchi pale wanapokuwa wanatimiza majukumu yao kwani kauli kama hizo ndizo zinazoleta mazingira ya kuomba rushwa ili mtu apate msaada.
Post a Comment