Lionel Messi atupwa jela miaka miwili kwa kushindwa kulipa kodi
Mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi
amehukimiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.
Baba yake, Jorge Messi, naye amehukumiwa kwenda jela kwa kukwepa kulipa kodi inayofikia dola milioni 4.5 kuanzia mwaka 2007 hadi 2009.
Pia wanakabiliwa na faini ya mamilioni ya euro kwa kuficha fedha nyingi huko Belize na Uruguay zilizotokana na mapato mbalimbali.
Hata hivyo, hakuna atakayeenda jela kutumikia kifungo hicho.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu chini ya miaka miwili inaweza kutumikiwa kwa uangalizi.
Mchezaji huyo pamoja na baba yake walipatikana na hatia ya makosa matatu ya ukwepaji kodi katika mahakama ya mjini Barcelona.
Pamoja na kifungo hicho, Messi alipigwa faini ya €2m na baba yake €1.5m. Walilipa kwa hiari jumla ya €5m sawa na kodi inayodaiwa hawakuilipa pamoja na riba, August 2013.
Hukumu hiyo inaweza kukatiwa rufaa kwenye mahakama kuu

Post a Comment