Hii ndiyo kamati mpya ya Miss Tanzania, Jokate Mwegelo ajumuishwa
Kamati mpya ya Miss Tanzania imetambulishwa rasmi leo August 27, 2015, na miongoni mwa wajumbe yumo Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu pamoja na Jokate Mwegelo ambaye ni msemaji wa kamati hiyo.
Mabadiliko hayo yamekuja wiki moja toka Baraza La Sanaa la Taifa, BASATA kulifungulia shindano hilo lililofungiwa kwa miaka miwili.
“Kwa niaba ya kamati mpya ya Miss Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya Lino International Agency Limited, kwa kutuamini na kututeua kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Miss Tanzania yenye majukumu ya kuandaa, kuratibu na kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.” Alisema msemaji wa kamati mpya Jokate Mwegelo.
“Tumekubali na tumepokea majukumu hayo na kuahidi kusimamia kanuni, sheria na taratibu za kuendesha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.Tunaomba jamii ya Watanzania watupe ushirikiano pamoja na kutuamini kwamba tunaweza kuisogeza mbele zaidi tasnia hii ya urembo hapa nchini” – Jokate Mwegelo.
Wiki iliyopita mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na East Africa Radio alikiri kuwa anafahamu watu wanahitaji mabadiliko katika mashindano hayo, hivyo akaahidi kuwa wataleta kamati mpya (Ingia hapa).
Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na wajumbe wafuatao:
1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi – Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi – Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
Wajumbe wa Sekretariet ni:
1.Dr.Ramesh Shah
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni
Post a Comment