Wewe huwa unafanya nini usiku kabla ya kulala? Hua unaangalia televisheni? Hua unatembelea tovuti na ndivyo jinsi ulivyoweza kupata tovuti hii? Au hua unatumia muda wako na familia yako?
Vipi kuhusu watu waliofanikiwa, huwa wanafanya nini kabla hawajalala? Hivi hapa ni vitu 10 ambavyo huwa wanafanya kabla ya kulala.

1. Hitimisha siku yako

Hufikia mahali na kusema sasa sehemu ya kwaza ya siku imekwisha na wanakwenda katika sehemu ya pili ya siku. Kama unafanya kazi hadi saa 12 jioni, hakikisha muda huo ukifika unakuwa umemaliza kazi za siku ili uingie kwenye upande wa pili wa siku yako. Hivyo kama uliahidi kupata chakula cha jioni na famili yako, hakikisha unatimiza.
Unatakiwa kupanga muda wako sawasawa siku nzima. Muda wa kulala, muda wa kufanya kazi na muda kwa ajili ya shughuli nyingine. Tayari umetumia muda wako mwingi kulala na kufanya kazi, hivyo basi, inapofika saa 12 au saa 1 jioni, tumia muda uliobaki kufanya mambo mengine katika maisha yako.

2. Kusoma Vitabu

Watu wengi waliofanikiwa duniani ni wasomaji wazuri wa vitabu. Wanasoma na kujifunza kutoka kwa wasemacho wengine. Unafahamu kuwa kwa kusoma na kujifunza kuna rahisisha kufanikiwa kwako? Ukweli ni kuwa mabilionea kama Bill Gates, huwa wanajisomea vitabu na makala sana na baada ya hapo ndipo hulala.
Matajiri wengi huhakikisha kuwa wanasoma kurasa kadhaa au kuwasomea watoto wao hadithi katika vitabu kabla ya kulala.

3. Hutumia muda mwingi na familia na marafiki

Ni kweli, mafanikio huanzia ndani. Inakubidi kutumia muda mwingi na familia na marafiki ili kuweza kuwa na ukaribu nao. Baadhi ya watu huamua kukutana na marafiki kila Jumatano,  na siku zilizobaki hukaa na familia zao. Ni suala na namna tu unavyopanga ratiba yako.

4. Jiweke tayari kwa siku inayofuata

Hiki ni moja kati ya vitu muhimu unavyopaswa kufanya kabla ya kulala. Panga kuhusu siku inayofuata, andika ni mambo gani ungependa kuyafanya siku inayofuata. Watu wengi hupiga pasi nguo zao na kuweka sawa vitu vyote ambavyo watavitumia kwa ajili ya siku inayofuata. Na wewe uwe unafanya hivyo.

Ukifanya hivi, utaamka ukijua ni kitu/vitu gani unapaswa kufanya kwa siku hiyo. Utakuwa makini na mwenye kufanya kazi kwa manufaa zaidi kwa sababu umejipanga na kila kitu kinakwenda sawa. Usipojiandaa kwa ajili ya siku inayofuata hakuna kitakachokwenda sawa, unaamka kwa kuchelewa, nguo hazijapigw pasi, huoni ulipoweka documents muhimu kwa ajili mkutano. Siku yako itakuwa ni mvurugano, hivyo ipange siku yako kabla ya kulala.

5. Jitenge na Dunia

Kuna wakati utataka kujitenga na kila kila kitu. Hii ni muhimu hasa kwa dunia hii ambapo imekuwa kama kijiji, unaweza kujiunga na mtu aliyeko popote na pengine akakukwaza. Simu yako inaweza kuita muda wowote kama hujaizima. Kuna wakati unahitaji kujitenga na kazi zako za kila siku na kunawakati unahitaji kuwa mwenyewe. Tafiti zinaonyesha kuwa wakati upo mwenyewe inakusaidia sana kupata muda wa faragha.

6. Tafakari (Meditation)

Moja ya kitu muhimu ambacho unaweza kukifanya usiku ni kutafakari. Tafakari ni nzuri kwa ajili ya afya ya akili yako pamoja na mwili. Hii husaidia kukupa nguvu upya na kukufanya uweze kuwa makini kwenye ufanyalo. Hukuburudisha baada ya mihangaiko ya siku nzima. Jifunze kufanya tafakari kabla ya kulala kwa ajili ya afya ya akili na mwili wako. Unaweza ukaifanya dakika tano au kumi kabla ya kulala.

7. Ifikirie kesho yako

Njia rahisi ya kujiweka tayari kwa ajili ya jambo lijalo ni kulifikiria. Ukifikiri kuhusu siku yako unaifanya inakuwa sawa, utakuwa umejiandaa na kukabili kila jambo litakalo kujia.

Tumia japo dakika tano kufikiri kuhusu siku inayofuata kabla ya kulala. Fikiri kuhusu kitu utakachokifanya kesho na namna ya kukifanya. Fikiri juu ya mtu utakayezungumza nae kesho na namna utakavyozungumza naye. Utakapokuwa ukifikiri, fikiri kwa namna ambavyo mambo yanakwenda sawa. Matatizo yote yanayoibuka fikiri kwamba umeyatatua, na hivi ndivyo unavyoweza kuwa na siku njema.

8. Orodhesha mambo uliyoyatimiza kwa siku

Ni mambo gani umeyatimiza/umeyakamilisha ndani ya sku yako? Baadhi ya watu watasema hakuna kwa sababu wanafikiri hawakuwa na siku yenye mafanikio
.
Unapofurahia kuwa ulikuwa na mlo kamili mchana, mlo kamili usiku, kuweza kufika nyumbani salama na kukaa na familia yako, utajisikia furaha sana ndani yako. Kwa upande mwingine, kama hutakuwa na furaha kwa hayo yote uliyonayo, utakua na stress, na kujiona sio mkamilifu.

Hivyo basi, andika japo mambo matatu ambayo unayapenda na umeyatimiza kwa siku kila siku usiku unapokua unajiandaa kwa siku inayofuata. Andika mafanikio yote makubwa na madogo uliyofanikisha. Hata kama ni kupiga simu, au ulisoma kitabu kwa dakika 5. Andika tu na ujifunze kukubali mafanikio madogo unayoyapata kwa siku.

9. Timiza majukumu yako

Utaanza siku inayofuata na viporo vya kazi? Unapojua kuwa una jambo moja hujafanya na tayari ni usiku, Je! Utaacha umalizie kesho? Hii inategemea na mtu na muda ambao kazi iliyosalia utatumia kuimaliza.
Watu wengi waliofanikiwa hutimiza wajibu wao kabla ya kulala. Wanajituma na kuhakikisha kila kitu ambacho ni muhimu kinakamilika kama walivyopanga kabla ya kulala. Mfano, kama kuna mteja ambaye inakupasa kumhudumia na tayari ni saa 12 au saa 1 jioni muda ambao unataka kufunga ofisi, kitu unachoweza kufanya ni kuwatumia ujumbe kwamba utawahudumia siku inayofuata. Kwa kiasi hili litasaidia kuondoa msongo wa mawazo na kuwafanya wateja wako kuona kuwa hujawapuuza.

10. Lala muda wa kutosha

Je! Huwa unapata muda wa kutosha kulala? Na unajua kuwa kulala muda wa kutosha ni njia moja ya kuupatia mwili wako nguvu kwa ajili ya siku mpya utakapoamka. Usipolala kwa muda wa kutosha utajihisi mwenye uchovu sana. Hautaweza kutimiza majukumu yako na kufanya siku yako iwe ya mafanikio kama utakuwa umechoka.