Jay Z afungua akaunti Instagram na kuifuta ndani ya saa 24!
Rapper Sean “Jay Z” Carter weekend iliyopita alijiunga kwenye mtandao wa Instagram, lakini cha kushangaza aliifunga akaunti hiyo ndani ya saa 24
Jigga alifungua akaunti kwa jina la ‘HovSince96’ siku ya Jumamosi August 29.
Picha aliyopost Jay Z kwenye akaunti yake ya Instagram
Kwenye akaunti hiyo alipost picha yake moya ya zamani aliyopiga na mfalme wa Pop, marehemu Michael Jackson na kuandika kuwa huenda hiyo ndio ikawa post yake ya kwanza nay a mwisho.
“Happy Birthday to the King! This may be my first and last post,” aliandika Jay Z
August 30 ilikuwa ni siku aliyozaliwa MJ, kama angekuwa hai angefikisha miaka 57.
Post a Comment