Mariah Carey akanusha uvumi kuwa ana ujauzito wa boyfriend wake bilionea
Mariah Carey amekanusha tetesi zilizosambazwa wiki hii na jarida moja kuwa ana ujauzito wa boyfriend wake wa sasa James Packer.
Mwakilishi wa Mariah ameuambia mtandao wa Just Jared kuwa taarifa hizo si za kweli.
Jumatatu ya wiki hii jarida la New Idea la Australia, lilidai kuwa Mariah na boyfriend wake bilionea James Packer ambaye ni mmiliki wa macasino nchini Marekani, wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza toka waweke hadharani uhusiano wao June mwaka huu.
“Mariah found out the baby news recently and they’re overjoyed at the prospect of being parents,” liliandika jarida hilo kwa madai kuwa lilimnukuu mtu wa karibu na Mariah.
James ni baba wa watoto watatu aliowapata na aliyekuwa mke wake wa zamani, na Mariah ni mama wa watoto wawili mapacha aliowapata na Nick Cannon ambaye waliachana mwaka 2014.
Post a Comment