Image result for tigo banner

Davido ni shabiki mkubwa wa Joh makini,athibitisha kwa hii tweet

joh davido

“Hii kusema kweli imeanza kitambo na mchizi alikuwa ananifatilia, nakumbuka mara ya mwisho kuna show moja ilifanyika kubwa Leaders (Fiesta) na mchizi alikuwepo, sasa wakati wa performance yangu na jamaa alikuwepo, sasa kuanzia pale jamaa alikuwa ananiulizia who is this guy watu wakawa wananiambia, yaani alikuwa surprised show ilikuwa kubwa…”
Ameongeza kuwa baada ya kupata feedback kutoka kwa watu mbalimbali kuwa Davido anamzungumzia vizuri na anatamani kufanya naye kazi aliamua kutumia fursa hiyo kuwasiliana naye kwaajili ya kufanya kazi.
“Sasa vitu kama hivi vinapokuja inabidi na wewe ujiongeze kidogo, tukamcheki kama kuna uwezekano wa kufanya kazi na mchizi, na mchizi mwenyewe akasema alikuwa anataka sana kufanya kazi na mimi”
Joh amesema kuwa tayari wameanza maandalizi ya kufanya wimbo huo licha ya Davido kuweka wazi mapema bila yeye kutarajia.
“Sema yeye nafikiri amekuwa na haraka sana kuipeleka kwenye media lakini sio mbaya.” alisema Joh.
Bado haijajulikana wimbo watakaofanya utakuwa ni wa nani, lakini Joh amesema inaweza ukawa wa wote wawili, lakini kazi ikishafanyika watafanya mazungumzo kuamua juu ya hilo.
Hii itakuwa ni collabo ya tatu ya kimataifa kwa Joh Makini kwa mwaka huu, baada ya ile ya AKA pamojan nay a K.O ambayo nayo bado iko kwenye maandalizi.

No comments

Powered by Blogger.