Alikiba apata shavu lingine la kimataifa
Wasanii mbalimbali wa Afrika leo wanaungana na wananchi mjini Kigali, Rwanda kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani.
Rwanda ni mwenyeji wa maadhimisho hayo barani Afrika.
Wasanii watakaotumbuiza kwenye maadhimisho hayo yanayofanyika kwenye uwanja wa Amahoro jijini Kigali ni pamoja na Alikiba, Ice Prince, Maurice Kirya, Lillian Mbabazi, Mafikizolo na Wangechi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni ‘Partnerships for Peace – Dignity for all.’
Mwaka 1994, Rwanda ilijikuta kwenye wakati mgumu kufuatia mauaji ya halaiki yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja wengi wao wakiwa watutsi
Post a Comment