Diamond aeleza alivyolipokea shavu la Swizz Beatz
Diamond Platnumz ni mtu mwenye furaha kubwa baada ya producer maarufu wa Marekani, Swizz Beatz kupost video mbili kwenye Instagram zikimuonesha yeye na binti yake, Nicole Dean wakisikiliza nyimbo zake.
Diamond ameiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM kuwa, baada ya kugundua Swizz amepost video hiyo, aliamua kupost picha akiwa na Ne-Yo studio ili kuionyesha dunia kuwa kuna mengi mazuri yanakuja kutoka kwake.
“Nilikuwa nipo studio narekodi,” amesema muimbaji huyo. “Kidogo nikaambiwa Swizz kapost wimbo wako. Nikaona kama ananitania! Nikaangalia kweli, kidogo nikaona jamaa kanifollow, nikasikia raha. Nikakaa, nikabidi nitumie ujanja. Ikanibidi nirepost picha moja nikiwa na rekodi na Ne-Yo ili kutengeneza mazingira anapo ni preview aone hawa jamaa wapo vizuri, kuna kolabo ya Ne-Yo karibu inatoka. Kukaa dakika mbili akapost Nataka Kulewa. Ikabidi ni repost Nataka Kulewa. Kwanza nilitaka nirepost Nana, nikasema nikirepost Nana wanaigeria wataona kama Swizz kasilikiza nyimbo kupitia Nigeria. Ndio maana nikarepost Nataka Kulewa ili kuwaonyesha wanaigeria ni muziki wa Tanzania unakubalika,” ameongeza.
“Kwa mtazamo wangu mimi naona muziki wa Tanzania unaendelea kufanya vizuri. Unaonyesha zaidi kwamba unakubalika. Unajua sisi tunaimba Kiswahili na nyimbo ambazo tunaimba Kiswahili hawazielewi, kwahiyo ukiona wanasikiliza ujue tumepiga hatua. Huu ni wakati wasanii kushirikiana ili kufikisha muziki wetu mbali.”
Post a Comment