Drake aweka rekodi nyingine Billboard
Huu umekuwa mwaka mzuri kwa Drake. Aliachia mixtape ya ushirikiano na Future, What a Time To Be Alive na sasa amefikisha nyimbo 100 kwenye chart ya Billboard Hot 100 tangu aanze kufanya muziki miaka sita iliyopita.
Rapper huyo anayetokea nchini Canada alikuwa na nyimbo 92 kabla ya mixtape yake kutoka Jumapili iliyopita ambapo nane kati ya 11 zilishika namba moja. Kwa mujibu wa Billboard, ni wasanii/makundi wa/manne waliofanikisha hilo tangu mwaka 1958 walipoanza kuweka rekodi hizo.
The Glee ndio ilikuwa na nyimbo nyingi kwenye Billboard Hot 100 (207), wakifuatiwa na Lil Wayne (127), Elvis Presley (108), na kisha Drake.
Mixtape yake na Future pia ilikamata No. 1 kwenye Billboard 200.
Pia rapper huyo anadaiwa kuwa mbioni kutoa album yake mpya, “Views From The 6” baadaye mwaka huu.
Post a Comment