Diamond atajwa kuwania tuzo zingine Nigeria, ‘The African Entertainment Legend Awards’ (AELA)
Diamond Platnumz a.k.a Baba Tiffah yuko kwenye orodha ya waliotajwa kuwania tuzo zingine za nchini Nigeria, ‘The African Entertainment Legend Awards (AELA)’.
Platnumz ametajwa kuwania vipengele viwili, ‘African Legends Artist of The Year’ akichuana na Dbanj, P-Square, Faze, Reggie Rockstone, Asa, R2bees pamoja na 2face.
Kipengele cha pili anachowania ni ‘Best collabolation’ kupitia wimbo wake ‘Nana’ aliomshirikia Flavour. Katika kipengele hiki wasanii anaowshindana nao ni Wizkid (Ojuelegba) ft Drake, Flavour (Sexy Rosey) ft Psquare, Davido (Fans Mi) ft Meek Mill, Sarkordie (New Guy) ft. Ace, Dbanj (Feeling The Nigga) ft. Akon, Kiss Daniel (Woju Remix) Ft Davido, Tiwa savage, Skepta, Harrysong (Reggae blues) ft. Olamide, Kcee,Orezi,Iyanya, Patoranking (My Woman) ft Wande coal.
Tuzo za AELA zitatolewa Novemba 11, 2015 jijini Lagos, Nigeria
Post a Comment