TFF yamfungia Juma Nyoso kucheza soka kwa miaka miwili
Kamati ya uendeshaji ya ligi kuu Tanzania Bara iliyokutana September 29 kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya ligi kuu na ligi daraja la kwanza nchini, imemfungia nahodha wa Mbeya City, Juma Nyoso kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili.
Pia imempiga faini ya shilingi milioni mbili kuafutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC, John Bocco.
Post a Comment