Dully Sykes aukana wimbo wake mpya ‘Kwani Wewe Ni Nani’
Dully Sykes amesema hategemei mafanikio yoyote kutoka kwenye wimbo wake mpya uitwao ‘Kwani wewe ni nani’.
Muimbaji huyo amesema wimbo huo sio rasmi na kwamba ngoma rasmi inakuja hivi karibuni.
“Nyimbo niliyoachia hivi karibuni siyo official, ni ya kwenye mitandano tu ili kila mtu awenayo katika mkono, sio kama eti hii nyimbo ipigwe redio wala nini,” alisema. “Siitegemei hiyo nyimbo iwe hit ili inipeleke kokote, na wala sijaruhusu ipigwe, ninayo single yangu mpya inakuja lakini sio hii,” Dully Sykes alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio
Post a Comment