Eddie Kenzo awapiku Diamond,Sauti sol na Sarkodie kwenye Nigeria Entertainment Awards’ 2015
Tuzo za Nigeria Entertainment Awards 2015 (NEA) zimetolewa usiku wa Sept .6 huko New York nchini Marekani, lakini safari hii bahati ya ushindi haikuwa kwa msanii wa Tanzania aliyekuwa akituwakilisha katika tuzo hizo.
Msanii wa Uganda, Eddie Kenzo ndiye aliyeibuka mshindi wa kipengele cha ‘African Artist of The Year’ ambacho kilikuwa ni maalum kwa wasanii wasio Wanigeria.
Wengine waliokuwa wakiwania kipengele hicho ni pamoja na Diamond, Sauti Sol (Kenya). Sarkodie (Ghana) na Stoneboy (Ghana)
Post a Comment