Gazeti la MwanaHALISI la rudi kitaani baada ya kushinda kesi
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk.
Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia
gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita.
Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.
Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.
Katika uamuzi wa shauri lililofunguliwa mara baada ya
MwanaHALISI kufungiwa, Jaji Bongole amesema gazeti hilo liko huru
kuchapishwa kuanzia sasa.
Jaji huyo amesema pamoja na uamuzi huo, kampuni
iliyolalamika imepewa mafao yote iliyoyaomba katika kufungua shauri hilo
la mapitio ya uamuzi wa Waziri – prerogative orders.
Miongoni mwa maombi ya faida ni HHPL kulipwa gharama za
kesi pamoja na fidia kutokana na hasara iliyopatikana kwa muda wote wa
gazti hilo kuwa kifungoni.
Wakati Waziri alipofungia gazeti la MwanaHALISI, alieleza kwamba sababu ni kuandika habari na makala za uchochezi.
Habari hasa iliyoikera serikali hata kujilazimisha kuchukua
hatua hiyo katili, ilikuwa ni iliyohusu uchunguzi wa tukio la kutekwa
na kuteswa hadi karibu na kifo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha
Madaktari Tanzania (TMA), Dk. Steven Ulimboka.
Dk. Ulimboka alikumbwa na mkasa huo mnamo Juni 2012
alipotekwa usiku eneo la Tazara, karibu na viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni, ambako aliitwa na mtu aliyemtaja kuwa ni ofisa wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, ambaye alikuwa na mawasiliano ya karibu naye kwa saa kadhaa
siku chache na usiku huo siku ya tukio.
Daktari huyo aliyekuwa mtumishi wa taasisi ya Marekani
nchini, alifika eneo la Tazara akifuatana na daktari mwenzake aitwaye
Deo, ambaye mara baada ya tukio hilo, wakati wa alfajiri, alimpigia simu
Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa, kumjulisha kuhusu kutekwa kwa
Dk. Ulimboka.
Kufuatia habari za kuachiwa huru kwa MwanaHALISI, Mhariri
huyo amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya Tanzania, kwa kuwa
umethibitisha kosa la serikali la kujichukulia maamuzi mkononi chini ya
kuvunja sheria ilizoahidi kuzilinda.
“NImefurahi sana kuthibitishiwa kwamba serikali ilikosea
katika kufungia gazeti. Uamuzi wa jaji umesema waziri hakufuata hatua za
kisheria alizopaswa kuchukua kabla ya kufungia gazeti, ikiwemo ya
kuwapa wamiliki na mhariri nafasi ya kujitetea,” amsema Idrissa.
“Lakini pia uamuzi huu unatakiwa uwe funzo muhimu kwa
utawala kwamba hauwezi kudumu na kudumu kwa msisitizo wa kuhifadhi na
kufurahia sheria zilizopitwa na wakati ambazo miaka kadhaa nyuma
zilishatangazwa kuwa ni sheria kandamizi,” alisema.
Mhariri amesema anawasiliana na mmiliki na mchapishaji wa
MwanaHALISI, kampuni ya HHPL, kukamilisha taratibu za kuchapisha toleo
la kwanza haraka iwezekanavyo. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa mara
moja kwa wiki siku ya Jumatano.
Post a Comment