Kim Kardahsian anatarajia kujifungua mtoto wake wa pili siku ya Christmas
Rapper Kanye West na mkewe Kim Kardashian ambaye ni mjamzito wanatarajia kumpokea mdogo wake na North siku ya Christmas, ambapo Kim ndio anatarajia kujifungua.
Kwa mujibu wa TMZ, Kim K anatarajia kujifungua mtoto wake wa pili Dec. 25. Vyanzo vya karibu vimedia kuwa couple hiyo tayari ime ‘book’ Deluxe Maternity Suite kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center iliyoko L.A, Marekani.
Hiyo ndio hospitali ambapo mtoto wao wa kwanza North West mwenye miaka miwili sasa pia alizaliwa.
Hivi karibuni Kim K kupitia Twitter alitangaza kuwa anatarajia kupata mtoto wa kiume.
Post a Comment