Mahujaji watano kutoka Tanzania ni miongoni mwa 717 waliopoteza maisha Mecca
Mahujaji watano kutoka Tanzania wamethibitishwa kuwa wamepoteza maisha huko Mecca baada ya kutokea mkanyagano katika siku ya mwisho ya Hijja. Takriban mahujaji 717 walifariki baada ya kukanyagana karibu na mji huo mtakatifu wa kiislam, Mecca uliopo nchini Saudi Arabia.
Taarifa hiyo imetolewa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abu Bakari Zuberi.
Watu wengine 863 walijeruhiwa kwenye tukio hilo lililotokea kwenye eneo la Mina, wakati ambapo mahujaji milioni mbili kutoka nchi mbalimbali duniani walikuwa kwenye siku ya mwisho ya Hijja.
Hilo ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha Hijja katika kipindi cha miaka 25.
Wakati wa Hijja, mahujaji walisafiri kwenda Mina, bonde kubwa lililopo kilomita tano kutoka Mecca, ili kwenda kurusha mawe saba kwenye nguzo za Jamarat.
Nguzo hizo zinaaminika kuwa sehemu ambayo shetani alimrubuni Nabii Ibrahiym.
“Tayari tumethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine wanne ni Watanzania,” imesema taarifa ya Mufti.
“Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni Bi Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla.
Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana hadi Alhamisi usiku wakati tukiandaa taarifa hii. Raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Bi Fatuma Mohammed Jama,” imeongeza.
Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana hadi Alhamisi usiku wakati tukiandaa taarifa hii. Raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Bi Fatuma Mohammed Jama,” imeongeza.
“Kuna taarifa ya mahujaji wanawake wawili ambao hadi Alhamisi usiku walikua hawajapatikana hivyo hatukua na uhakika juu ya usalama wao hadi tutakapowaona ama kupata taarifa zao.
Ifahamike kuwa majina yamepatikana kupitia vitambulisho vyao ambavyo wahanga wa tukio hili waliweza kuvichukua kutoka kwenye miili ya marehemu. Nimepokea taarifa za majeruhi miongoni mwa mahujaji wetu wa Tanzania na baadhi ya majeruhi hao nimeonana nao mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.”
Ifahamike kuwa majina yamepatikana kupitia vitambulisho vyao ambavyo wahanga wa tukio hili waliweza kuvichukua kutoka kwenye miili ya marehemu. Nimepokea taarifa za majeruhi miongoni mwa mahujaji wetu wa Tanzania na baadhi ya majeruhi hao nimeonana nao mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.”
“Vilevile nimeagiza maafisa wetu wa Bakwata nilionao hapa Mina kuendelea kufuatilia habari na taarifa za mahujaji wetu katika hospitali na sehemu za kuhifadhia maiti. Nimefanya hivyo ili niweze kuwa na uhakika juu ya usalama wa mahujaji wetu,” imesisitiza taarifa hiyo.
“Katika kipindi hiki cha taharuki kubwa tunafanya mawasiliano na wizara husika hapa Saudi Arabia kwa kushirikiana na serikali yetu kupitia ubalozi wetu hapa Saudi Arabia. Natambua uwepo wa mkanganyiko wa taarifa ambazo zinazidisha taharuki kwa ndugu na jamaa wa mahujaji wetu. Nachukua fursa hii kuwaomba ndugu na jamaa wa mahujaji kuwa watulivu na kuwa na subra katika wakati huu mgumu sana kwetu sote.”
“Tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana na Insha Allah mara tu tukipata taarifa za uhakika basi tutawafahamisha. Kutokana na idadi ya maiti kuwa kubwa serikali ya Saudi Arabia wanaendelea na zoezi la kutambua uraia wa kila mwili ili waweze kutoa taarifa tunatarajia wakati wowote tutakuwa tumepata taarifa zaidi.”
Tukio hilo limetokea wiki chache tuu baada ya watu 109 kupoteza maisha baada ya kuanguliwa na cranes kwenye msikiti mkuu wa Mecca
Post a Comment