Image result for tigo banner

Navy Kenzo watumia 80% ya malipo ya show kufanya maandalizi ya show hiyo

Ili msanii afanikiwe anahitajika awe mwepesi katika kuwekeza katika kazi zake ili kujiongezea thamani ya kazi yake.
navy kenzo
Wapo wasanii wengi ambao wanajinyima kufanya starehe na mambo mengine ya kimaisha ili wawekeze katika kazi pesa wanazopata kwenye shows pamoja na vipato vingine.
Nahreel amesema kuwa yeye na Aika wanaounda Navy Kenzo walitumia asilimia 80 ya pesa walizolipwa kwenye show ya Kilifest iliyofanyika Jumamosi iliyopita viwanja vya Leaders, kwaajili ya maandalizi ya show hiyo ili kuwapa mashabiki show bora na kuongeza thamani yao.
“Sasa hivi tumeamua kuinvest kwenye show, hii show imetucost kama milioni 5 kuandaa kila kitu, tumelipwa vizuri. Tuseme kama asilimia 80, unajua muziki ukitaka ukurudishie lazima uwekeze”. Alisema Nahreel kupitia 255 ya XXL

No comments

Powered by Blogger.