Image result for tigo banner

Roma asema hajapewa barua rasmi ya kufungiwa wimbo wake na BASATA

Rapper Roma Mkatoliki ameendelea kutawala vichwa vya habari kufuatia sakata la kufungiwa kwa wimbo wake wa Viva Roma Viva.
roma new pic
Akizungumza kupitia Planet Bongo ya E A Radio, Roma amesema kuwa yeye binafsi hajapokea barua rasmi ya kufungiwa wimbo wake kutoka BASATA.
“Sina jibu la moja kwa moja na napata kigugumizi kwa sababu sina taarifa rasmi kwa kweli, yani finaly mimi nakuwa kama shabiki tu tena, vile shabiki alivyoona ndivyo mimi kama Roma nilivyoona, niliamka tu na mimi nikaona kama kuna chombo kimoja cha habari kimepost katika akaunti ya Instagram, kwamba kuna tamko limetoka BASATA kwamba limefungia nyimbo ya Roma, kwa sababu ambazo walizianisha”.
Aliongeza kuwa yeye hajui utaratibu ambao BASATA inautumia kufikisha taarifa kama hizo kwa wasanii.
“Nisiwe muongo sijui taratibu kinakuwa kinatumia kufikisha information zao, kwa sababu kitu ambacho naona ingekuwa rahisi kama artist kabla hajaachia nyimbo yake mpya ama hajafanya kazi yake ya sanaa, iwe inawasilishwa katika hiko chombo, nadhani hapo tungekuwa tunaenda sawa.”
Upande wa Afisa Habari wa BASATA, Bwana Aristide Kwizela, alisema kuwa zipo njia mbili ambazo wanaweza kutumia kutoa taarifa za namna hiyo.
“Kuna kufungia kwa maana ya msanii mwenyewe kuandikiwa, lakini kama kuna taarifa imetoka public kwamba nyimbo za namna hiyo zimezuiliwa, kuna two way either barua kuandikwa kwa msanii au pia kuna public anouncements kwamba wimbo fulani umefungiwa”, alisema Kwizela.

No comments

Powered by Blogger.