Picha: Vanessa na Jux washoot video mpya Afrika Kusini
Vanessa Mdee na Jux wameungana na muongozaji wa Afrika Kusini, Justin Campos kwa mara nyingine tena kushoot video zao mpya.
Kwa kuangalia picha walizoweka kwenye Instagram inaonesha kuwa pamoja na kuwa pamoja jijini Jozi, kila mmoja anashoot video yake mwenyewe.
Kwenye picha picha moja aliyoweka Jux kwenye Instagram anaonekana akiwa amemshika mkono Vanessa huku stylist aitwaye Mchustle akimtengeneza kiatu. “Day 1 and still my A 1 #bad #mchustlestyling,” ameandika Jux.
Kwenye picha nyingine hiyo juu ambayo Jux amepost picha ya gari la kifahari litakalotumika kwenye video yake na ameandika: My baby for a night #africanboy.”
Muongozaji wa video hiyo, Justin Campos akiwa kwenye gari la video ya Jux
Post a Comment