Wiz Khalifa alifundishwa na mama yake kuvuta Bangi
Wiz Khalifa ni Rapper ambaye ni mzazi mwenzake na Mwanamitindo Amber Rose,
wote ni mastaa wenye majina makubwa Duniani… Kuna Majimbo Marekani
wameruhusu Bangi kuwa kilevi halali kabisa lakini kwingine ni MARUFUKU
!!
Wiz Khalifa
huwa anaonekana anavuta kuanzia kwenye Video zake, pichaz… hii kitu kwa
jamaa ni kama tu sehemu ya maisha yake ya kawaida kabisa >>> ‘Alikuwa
akisikia harufu kutoka chumbani kwangu ambapo mimi na marafiki zangu
tulikuwa tunavuta… alihisi ni kitu kizuri kwa vile kila wakati alisikia
vicheko pamoja na harufu kali kutoka chumbani‘– Hii ni moja ya nukuu kwenye alichokisema Katie ‘Peachie’ Wimbush-Polk, mama wa Rapper Wiz Khalifa.
Hii ndio sentensi ya mama yake kuthibitisha kwamba tabia ya kuvuta Bangi alimfundisha yeye >>> ‘Kabla
sijaenda kazini, na yeye (Wiz Khalifa) hajaenda Shule ilikuwa ni lazima
tuvute pamoja… Alijifunza kuvuta kutoka kwa mama yake‘— Katie Wimbush-Polk.
Hapo ni Wiz Khalifa, mama yake mzazi Peachie-Wimbush na mtoto wa Wiz, Sebastian
Kwenye pesa ambayo Rapper huyo
anaingiza, kiasi ambacho anakitumia kila mwezi kwa ajili ya Bangi tu ni
Dola 10,000 ambazo ukiziweka kwenye hesabu ya Shilingi ni kama Ths.
Milioni 21 hivi !!
Post a Comment