Majambazi waivamia nyumba ya Nay wa Mitego
Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo walivamia nyumbani kwa Nay wa Mitego.
Nay ambaye yupo mikoani kwa sasa katika kampeni za siasa, ameiambia Bongo5 kuwa hana ugomvi na mtu yoyote na tukio hilo limemwacha kwenye dillema.
“Kuna watu walivamia nyumbani kwangu,” Nay ameiambia Bongo5.
“Ni usiku wa kuamkia jana, walikuwa wamevaa mask na walikuwa wanahangaika kukata nyaya za fensi ya alarm wakashindwa ndio wakaamua kupanda juu ya mstimu ili wakate umeme nyumba nzima. Lakini nashukuru Mungu majirani wakapiga kelele wakakimbia,” amesema.
“Sina ugomvi na mtu yoyote na siwezi kusema kwamba wametumwa. Tayari nimeshatoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea ila nasikia walikuwa na gari aina ya Land Cruiser nyeusi ambayo haikuwa na plate number.”
“Nashukuru Mungu familia yangu ipo salama na nimeongeza usalama zaidi.”
Post a Comment