Image result for tigo banner

Tyga aapa kuwa hatakuja kuvuta bangi mbele ya mwanaye

Rapper Tyga ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aliyempata na aliyekuwa mpenzi wake Blac Chyna.
Tyga-and-King-Cairo-Easter-day
Katika kuonesha kuwa yeye ni baba bora na mwenye malezi mema kwa mtoto wake aitwaye King Cairo, rapper huyo ameapa kuwa kamwe hatawahi kuja kuvuta bangi mbele ya mwanaye mwenye miaka mitatu, wala kuruhusu mtu mwingine yeyote kufanya hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya TMZ.
Tyga snapchat
Kauli hiyo imekuja baada Tyga kupost video controversial ikimuonesha mwanaye akiwa anacheza karibu na meza ambayo inaonekana kuna kitu kinachodaiwa kuwa ni msokoto wa bangi.
Video hiyo iliibua hisia tofauti kutoka kwa followers wake walioanza kuhoji uwezo wake wa malezi bora kwa mtoto huyo

No comments

Powered by Blogger.