Image result for tigo banner

Hii ndio filamu ya Bongo iliyouza zaidi kwa mujibu wa Steps Entertainment

Kampuni ya usambazaji wa filamu nchini, Steps Entertainment imesema licha filamu nyingi kushindwa kufanya vizuri sokoni katika kipindi hiki, filamu ya ‘Wake Up’ imeweza kufanya vizuri zaidi.
11796346_858648140856198_5910047054412595256_n
afisa masoko wa Steps, Kambarage alisema filamu hiyo iliyochezwa na mastaa mbalimbali imeweza kuhimili changamoto mbalimbali zilizopo kutokana mastaa zaidi ya 13 kuigiza katika ya filamu hiyo.
“Hali sio nzuri ukifikia kuuza nakala 10,000 lazima ushangilie na ni filamu ya Wake Up peke yake ambayo pamoja na changamoto zote imeweza kufanya vizuri sokoni. Lakini yote ni kwa sababu kuna wasanii 13 wakubwa ndio wamecheza hii filamu, yupo Mzee Majuto, Wolper, Irene Paul, Gabo, Hemedy Suleiman, Yusuf Mlela, Mabeste na wengine wengi tu,” amesema. “Hii pia imeuza kutokana na story kuwa nzuri na sio nyepesi nyepesi ndio maana tumekuwa tukiongea na producer kujaribu kuandika story nzuri ambazo hata soko likiwa baya lakini zitauza kutokana na ubora wake,” alisema Kambarage

No comments

Powered by Blogger.