Image result for tigo banner

Sio kwamba kila msanii wa nje tutampapatikia kufanya naye collabo – Joh Makini

Ni karibia saa 24 toka mashabiki wa muziki wa Afrika waishuhudie kwa mara ya kwanza video ya wimbo mpya wa rapper wa Tanzania Joh Makini ‘Don’t Bother’ ambayo kamshirikisha rapper wa Afrika Kusini AKA iliyotambulishwa kwa mara ya kwanza na MTV Base Nov.10.
Johmakini.1
Ni wazi kuwa collabo hiyo itawasaidia Joh Makini na AKA kuongeza mashabiki wapya kutokana na kwamba wote ni wasanii wakubwa kwenye nchi zao na tayari wana fanbase kubwa, lakini Joh Makini pia ametoa maoni yake juu ya mitazamo ya watu wengi ambao huamini kuwa collabo kama hizo ndio vigezo vya ukubwa wa msanii.
“Tumeshafanya kazi na watu wengi lakini unajua pia sio lazima sana sisi tufanye kazi na wasanii wa nje ndio tuonekane sisi ni wakubwa” alisema Joh kupitia 255 ya XXL.
Joh ametolea mfano wa ngoma yake iliyopita ‘Nusu Nusu’ ambayo hajamshirikisha msanii yeyote wa nje zaidi ya G-Nako kwenye kiitikio.
“…kwasababu ‘Nusu Nusu’ sina msanii wa nje mle ndani na ngoma inafanya vizuri, kwahiyo sio kwamba kila msanii wa nje si tutampapatikia kufanya naye collabo, inategemea na feeling na aina ya msanii mwenyewe.”
Video ya ‘Nusu Nusu’ iliyofanywa Afrika Kusini na Justin Campos imeshika chati mbalimbali za vituo vikubwa vya runinga Afrika.

No comments

Powered by Blogger.