Yemi Alade aweka rekodi mpya ya Youtube
Baada ya P-Square kuweka rekodi ya kuwa wasanii wa kwanza wa Nigeria kufikisha views milioni 30 Youtube kupitia video yao ya ‘Personally’ mwezi November 2014, na baadaye kuivunja rekodi yao wenyewe kwa video hiyo kufikisha views milioni 40 mwezi April 2015, msanii Yemi Alade naye ameweka rekodi kama hiyo kwa wasanii wa kike.
Yemi Alade ameweka rekodi mpya kwa kuwa msanii wa kwanza wa kike wa Nigeria kufikisha views milioni 30 kupitia hit yake ‘Johhny’ iliyomtambulisha sehemu nyingi ikiwemo Afrika Mashariki. Hadi sasa video hiyo ina views 30,199,702.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Shaa ndiye anashikilia rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kufikisha views zaidi ya milioni 20 kwenye mtandao wa Youtube kupitia video ya wimbo wake ‘Sugua Gaga’ iliyoko kwenye channel ya Seka Moke. Hadi sasa ina views 20,429,726.
Post a Comment