Belle 9: Mimi sina tatizo na Diamond, ni baada ya kutokea sintofahamu instagram.
Watu wasiyo julikana wamehack akaunti ya facebook ya msanii Belle 9 na kuweka post yenye picha ya msanii Diamond na kuandika maneno yanayoashiria matusi ya nguoni.
Belle 9 amesema yeye anajulikana sio msanii wa kufanya vitu kama hivyo.
“Mimi sina tatizo na msanii wala sina upande wowote,” alisema Belle 9.
“Hili ni tatizo kama matatizo mengine, ni geni kwangu kwa sababu halijawai tokea lakini kwa wasanii wengine yalishatokea. Kwa hiyo naweza sema bado watu wangu wanaendelea kurekebisha tatizo na kuirudisha akaunti yangu. Mimi naimani kuwa watu wameelewa kuwa sio mimi kwa sababu mimi sio mtu wa mambo hayo,” aliongeza Belle.
Post a Comment