Harmonize ashika nafasi ya kwanza chati za video Sound City

Ni ukweli usiopingika kwamba bongo fleva kwa sasa inafanya vizuri nje ya nchi. hivi karibuni tumejionea wasanii kama Diamond, Navy Kenzo na wengine wengi kutoka Tanzania wakiongoza chati za vituo vikubwa vya Television Afrika ikiwemo MTV na Sound City. Sasa ni zamu ya Harmonize kutoka lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz. Harmonize kwa sasa ndiye anayeongoza chati za Sound City akiwa ameshikilia nafasi ya kwanza.
Post a Comment