Mabaki ya ndege ya EgyptAir yapatikana
Jeshi la Misri na
shirika la safari za ndege nchini humo zimesema kuwa mabaki ya ndege ya
EgyptAir iliotoweka yamepatikana katika bahari ya Mediterranean.
Msemaji wa jeshi la Misri alisema kuwa mabaki na abiria wa ndege hiyo walipatikana kilomita 290 kutoka mji wa Alexandria.
Katika taarifa yake, Rais Abdel Fattah al-Sisi alisikitishwa na ajali hiyo.
Kampuni ya ndege ya EgyptAir pia ilithibitisha kupatikana kwa mabaki hayo katika mtandao wake wa Twitter.
Ugiriki inasema kuwa rada yake imekuwa ikionyesha kwamba ndege hiyo iligeuka kwa ghafla mara mbili na kuanguka kutoka futi 25,000 na kuingia katika maji.
Post a Comment