Bajeti ya kwanza ya serikali ya Rais Magufuli 2016/17 kuwasilishwa leo Bungeni
Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mchana anatarajiwa kuwasilisha bungeni bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 ambao utaanza Julai Mosi.
Waziri Dkt. Philip Mpango ataiwasilisha bajeti ya serikali leo mchana huku wananchi wakiwa na kiu ya kutaka kujua vyanzo vipya vya mapato bya serikali ya awamu ya tano.
Hii ni bajeti ya kwanza ya serikali iliyo chini Rais Magufulu hivyo mamia ya watu nje na ndani ya nchi wanatamani kuisikia bajeti hiyo itakuwa ni ya namna gani. Je! Bajeti hii itatoa picha ya Tanzania ya viwanda?
Mbali na Tanzania, nchi ningine za Afrika Mashariki zinazosoma bajeti zao leo ni pamoja na Rwanda, Uganda na Kenya.
Post a Comment