Fahamu vishimo vilivyopo nyuma ya mgongo na maana yake kwa mwanamke
Kuna rafiki yangu mmoja katika maongezi tukaongelea kuhusu muonekano
wa vishimo hivyo vya nyuma ya mgongo na akanambia kwa mila zao wanaamini
ukiwa na vishimo hivyo mwanamke basi hautapata matatizo wakati wa
uzazi, kwa imani yake. Sasa turudi katika mada husika,nikiongelea
Dimples simaanishi Ommy Msanii Bali dimples kama Dimples au tunaita
vishimo, wengi wetu tuna vifahamu vile vilivyopo kwenye mashavu ya watu
ila, leo naongelea Dimples Katika Kiuno juu kidogo ya makalio.
Dimples
hizi au vishimo huwa kwa watu wa jinsia zote wanawake na kwa baadhi ya
wanaume, zinatambulika kama “Dimples of Venus” pia zinapewa majina
mengine mengi inategemea na jamii Fulani za watu, kwa wengine hii ni
ishara ya urembo ila kwa jamii zingine wanaona tu kawaida kama watu
wengine.
Kitu
usichojua juu ya dimples au vishimo hivyo ni vitu vya kurithi hii ikiwa
na maana kama jamii yako au ukoo wako hauna hivyo vishimo basi huwezi
tu kuvipata kiraisi, kama haipo katika vina saba (genes) zako basi si
vya kutengeneza japokuwa wanasema unaweza fanya mazoezi kupata vishimo
kama hivyo.
Labda
niongelee maana ya vishimo hivi kitu cha kwanza ni Mvuto/Urembo Baadhi
ya watu wanaamini kuwa ukiwa na vishimo hivyo unakuwa na mvuto hasa wa
kimapenzi na kwa wanawake wenye vishimo hivi kuwa wazuri pia faragha
yaani wanayaelewa mambo, wapo wanaume wanaosema wanavutiwa na vishimo
hivyo hasa wakiwa faragha.
Kitu
kingine Mtu akiwa na vishimo hivi ni dalili pia za afya bora yaani huna
uzito uliopitiliza wala kuna manyama uzembe hii pia inatokana na aina
ya mifupa yako mwilini, (Born structure) kila mtu anajinsi yake mifupa
inakaa katika mwili wake. kwahiyo wengine husema watu wenye vishimo
(Dimples) hizo ni watu wa pekee (special).
Imeandikwa na Rabiadamary.
Post a Comment