HII NDIO HUKUMU ALIYOPEWA ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI HII HAPA
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mkoa Wa Arusha,imemhukumu Isack Habakuki(40) mkazi Wa
Olasiti, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi
milioni 7 kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao wa
facebook.
Mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo na amekubali kulipa faini ambapo
mahakama imeamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili. Katika awamu ya
kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi
kilichobaki cha sh mil 3.5.
Isack anayeishi Kata ya Olasite, anadaiwa kutoa lugha ya matusi na
dhihaka kwa Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na
alikamatwa Machi 23, mwaka huu mjini Arusha na kupelekwa Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kisha alirejeshwa tena Arusha
Aprili 14, mwaka huu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile, Wakili wa Serikali, Gaudensia
Massanja, alidai kuwa Isack alikuwa akikabiliwa na kosa moja ambapo kwa
kufahamu na kwa makusudi mtuhumiwa huyo alitumia mtandao wa Facebook
kwa nia ya kumtukana Magufuli.
Alidai kwamba mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia
maneno yanayosema: “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu
bwege na Nyerere wapi buana.
Post a Comment