Hizi ndizo sababu sita za wapinzani kumng'oa naibu spika (TULIA ACKSON )
Wabunge wa upinzani wameendelea kususia kwa siku ya tatu mfululizo vikao vya Bunge vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson tangu walipotangaza hatua hiyo Jumatatu wiki hii kwa kutokuwa na imani naye.
Tangu Jumanne wiki hii wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo kwa madai kuwa anaminya demokrasia.
Siku hiyo wabunge hao waliingia bungeni kama kawaida na Dk Tulia
alipomaliza tu kusoma dua ya kuliombea Bunge, walitoka hadi kipindi
hicho kilipomalizika na naibu spika kumwachia mwenyekiti wa Bunge,
Andrew Chenge kuongoza, ndipo wote waliporudi ukumbini na kuendelea na
shu ghuli zao kama kawaida.
Juzi, wabunge hao wote kama kawaida waliingia bungeni asubuhi na
alipoingia Dk Tulia kuongoza kikao hicho, walisimama na kusikiliza dua
ya kuliombea Bunge, kisha walitoka na kuwaacha wabunge wa CCM
wakiendelea na Bunge.
Siku nzima ya juzi ambayo Dk Tulia aliendesha kikao cha asubuhi na
jioni, wabunge hao hawakuhudhuria na ilipofika wakati wa kusoma hotuba
ya msemaji wa kambi ya upinzani kwa Wizara ya Fedha na Mipango, David
Silinde aliingia ukumbini akitokea nje na kuomba hotuba yake iingie
kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge kama ilivyo. Kisha akasema: “Sitaisoma
hapa kwa kuwa haturidhishwi na mwenendo wa Naibu Spika wa kutuendesha
kama watoto.”
Wabunge hao wa upinzani walitoa sababu sita kwanini wanataka Dk Tulia aondolewe madarakani kwa Azimio la Bunge.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya wabunge hao, Mbunge
wa Simanjiro, James Millya alizitaja sababu hizo kuwa ni kwanza
1- Dk Tulia ameweka maslahi ya chama chake cha siasa mbele kuliko maslahi ya Bunge, kinyume na Kanuni ya 8(b) ya Bunge.
2- Mei 6 alitumia vibaya madaraka ya kiti cha Spika kwa kutoa uamuzi wa
mwongozo ambao ulikuwa unakiuka Ibara ya 12(2) ya Katiba. Muongozo huo
uliokuwa unapinga udhalilishaji wa wabunge wanawake,” alisema.
3- ni kitendo cha Dk Tulia kuvunja Kanuni ya 64(1) (f) na (g)
zinazokataza mbunge kutumia lugha ya matusi kwa mbunge mwingine ambapo
alinukuliwa akisema “Mheshimiwa Bwege, usionyeshe ubwege wako humu
ndani.”
4- ni Mei 30 kiongozi huyo aliamua kwa makusudi kuvunja Ibara ya 63(2)
ya Katiba na kutumia vibaya Kanuni ya 69(2) na 47(4) ya Kanuni za Bunge
kumzuia Joshua Nassari kwa upande mmoja na Bunge zima kwa upande wa pili
kutimiza majukumu yake ya kikatiba ya kusimamia na kuishauri Serikali.
5- ni kuwa Mei 26, mwaka huu Dk Ackson akiongoza kikao cha Bunge bila
ridhaa ya upinzani alishiriki kufuta sehemu ya hotuba ya msemaji wa
upinzani kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kinyume cha kanuni
ya 99(9) ya Bunge bila kushirikisha kamati yoyote ya Bunge,” alisema.
6- Millya alisema kuwa ni kitendo cha Dk Ackson kukataa taarifa ya maoni tofauti, iliyowasilishwa na wabunge wanne wa upinzani.
Post a Comment