Image result for tigo banner

Mbwana samatta awakatisha tamaa mashabiki wa taifa stars

Timu ya taifa ya Misri imekata tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon, baada ya kuwafunga wenyeji, Tanzania mabao 2-0 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
5R5A8408
Kwa matokeo hayo yanawafanya Misri wamalize mechi za Kundi G wakiwa na pointi 10 baada ya mechi nne, wakishinda tatu na kutoa sare moja, wakati Tanzania inabaki na pointi yake moja na inashika mkia nyuma ya Nigeria yenye pointi mbili.
Mohamed Salah alifunga mabao yake katika dakika ya 44 na 58 na kuikatisha tamaa kabisa Stars na mashabiki wengi waliojitokeza kuishangilia timu yao ya taifa.
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alikosa penalti baada ya Himid Mao kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

No comments

Powered by Blogger.