Image result for tigo banner

Naibu Spika Tulia azidi kuchapa kazi bila upinzani

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea na vikao vyake kama kawaida Mjini Dodoma ambapo wabunge wa kambi ya upinzani wameendelea na ajenda yao ya kutoka nje kila siku ambapo Naibu Spika Tulia Ackson ataongoza kikao cha Bunge.

Mapema asubuhi muda wa bunge saa tatu asubuhi wabunge walikuwa tayari ndani ya ukumbi wa bunge ambapo shughuli zimeanza kwa Dua ya kuliombea Bunge ambapo Naibu Spika Tulia ndiye alikuwa anaongoza shughuli za Bunge.

Baada ya Dua Naibu Spika amemtaka Katibu wa Bunge kutaja kazi zinazoendelea ambapo katibu amesema ni kipindi cha maswali, ambapo wabunge wote wa upinzani wakanyanyuka na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Baada ya kutoka nje shughuli za Bunge zimeendelea kama kawaida kwa wabunge wa Chama tawala CCM kuendelea kuuliza maswali na kupata majibu kutoka serikalini.

Msimamo huu wa wabunge wa upinzani unatokana na ajenda waliyopitisha kwamba siku Naibu Spika wa Bunge Tulia Mwansasu ataongoza kikao wabunge wote wa upinzani watatoka nje kwa shinikizo la kutokuwa na imani naye.

Hapo jana Naibu Msemaji wa wa Wizara ya Fedha David Silinde alikataa kusoma maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo kwa kigezo kwamba upinzani hauna imani na Naibu Spika wa Bunge na kuomba maoni yao yaingie kwenye kumbukumbu za Bunge.

No comments

Powered by Blogger.