Image result for tigo banner

Tunapendwa na wanawake- Diamond Platnumz

Wasafi Raymond, Rich Mavoko, Diamond Platnumz, pamoja na Harmonize
Diamond Platnumz akizungumza katika show ya Friday Night Live #FNL alisema inakuwa ngumu wao kama viongozi kuingilia maisha ya msanii kuhusu mahusiano yake kwani hayo ni maisha ya msanii binafsi bali wao kikubwa wanaangalia utendaji wa kazi na kuakikisha wanaleta kazi nzuri kwa jamii, na kusema wanatambua kuwa wanapendwa sana na watoto wa kike.

"Sisi tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu kwanza tunabahati ya kupendwa na tunajua hilo, hivyo msanii anapokuwa amezimiwa na mtu hatuwezi kumkataza kwani sisi kazi yetu ni kusimamia kazi za msanii na muziki wake na si kumsimamia msanii kwenye maisha yake ya mapenzi, maana ukimkataza msanii kutoka na mtu anayempenda ipo siku atajiongeza kwa mkeo pia. Lakini sisi tunajitahidi kufanya kazi kwa bidii sana tulete ngoma kali, video kali na show kali kwani ndiyo vitu vinavyofanya watu watukubali" alisema Diamond Platnumz

No comments

Powered by Blogger.