Image result for tigo banner

Uchambuzi: Kosa alilofanya muongozaji wa video ya Rich Mavoko "Ibaki Story"



“2 june” ime trend sana katikati ya wiki hii kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya mitandao mikubwa Tanzania ikiwemo bongo5.

kila mtu alikua akijiuliza nini kinakuja ghafla likaanza kuonekana tangazo hilo kwenye akaunti Za WCB wakishare bila kuandika chochote. 2-June ikafika na ndipo WCB wakategua kitendawili hicho na kumtambulisha Rich Mavoko kuwa msanii mpya kwenye label ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz ikifuatiwa na ujio wa video na Audio mpya ya msanii huyo inayoitwa ‘Ibaki Story’.

Lakini hapa nataka kuongelea kitu kidogo nilichokiona ndani ya video hiyo.

Story inaanza mpenzi wa Rich Mavoko (Video Model) akiondoka na kwenda kwa mwanaume mwingine lakini huko alikokukimbilia hali haikuwa shwari na kuanza kumkumbuka Mpenzi wake wa zamani (Rich Mavoko).

Mwanamke anaingia Maktaba na kumuona mtu kama Rich Mavoko na Ghafla kabla hajagundua mtu huyo ni nani mtu huyo anatoweka machoni mwake na ndipo anapoanza kumfwata nyuma na mwisho wa siku anamkuta kwenye ATM mashine na ndipo anagundua kuwa alikua amefananisha.
Director amefanya kazi nzuri lakini kuna kosa dogo ambalo amelifanya.

Scene iyamuonesha mtu aliyefananishwa akiwa maktaba

 
Mtu aliyemuweka Maktaba ili aonekane amefananishwa na Rich Mavoko ni Rich Mavoko mwenyewe huku akiwa amevaa hereni na ana ndevu ndefu huku nguo na vingine vinavyoweza kumtambulisha mtu kwa haraka vikiwa vipo sawa.

Scene ya pili mtu yule yule aliyeonekana maktaba sasa yupo ATM

Tukija kwenye scene ambayo anakuja kugundua mtu huyo si Rich Mavoko director alishindwa kuwafananisha mtu wa awali (Rich Mavoko) na aliyefananishwa ambaye mwanzo alionekana amevaa herein na ana ndevu lakini huku hana hereni wala ndevu na pia akiwa na muonekano tofauti wa nywele ukilinganisha na picha ambayo yupo maktaba. Hapo ndipo kosa lilipo , tukiachana na hayo video ni nzuri color grading ipo vizuri na stori imeendana na wimbo husika pongezi kwa management yake mpya WCB.

itazame video hiyo:
 

No comments

Powered by Blogger.