Agizo la waziri mkuu Majaliwa kwa mawaziri wote Tanzania
Kila ifikapo July 25 ya kila mwaka
Tanzania huadhimisha siku ya mashujaa ikiwa kwa mara ya kwanza July 25
2016 maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa katika mkoa wa Dodoma ambapo
pia mgeni rasmi alikuwa Rais John Pombe Magufuli akisindikizwa na viongozi wengine akiwemo Waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Majaliwa
alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi ambapo moja ya sentensi zake
ilikuwa ni agizo alililitoa kwa mawaziri wote kuhamia Dodoma ikiwa ni
kuanza kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli kutaka serikali kuhamia mkoani
humo.
‘Natoa
maagizo kwa mawaziri wote wahakikishe wanahamia mara moja Dodoma
kwakuwa najua wana nyumba za kuishi hapa lakini pia nimetoa maagizo
nyumba yangu imaliziwe nitahamia Dodoma mwezi wa tisa mwaka huu ‘ –Waziri mkuu Kassim Majaliwa
‘Sasa huu ndio wakati wenu Dodoma kujiandaa kwani hizi ni fursa za kukamata pindi serikali ikihamia hapa‘ – Waziri mkuu Kassim Majaliwa
Post a Comment