Uteuzi mwingine alioufanya Rais Magufuli leo July 25 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt.
Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la
Taifa (NDC).
Taarifa ya
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi huu
umeanza July 20 2016. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Samuel M. Nyantahe
alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI). Dkt.
Samuel M. Nyantahe anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Chrisant
Majiyatanga Mzindakaya ambaye amejiuzulu wadhifa huo.
Post a Comment