Image result for tigo banner

2face kuja na kitabu chake ‘A Very Good Bad Guy’

September 18, msanii nguli wa Nigeria, 2Face Idibia atatimiza umri wa miaka 40.
2Face-Idibia
Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, 2Face atafanya party ya nguvu iliyopewa jina ‘Fortyfied’ itakayojumuisha tamasha kubwa la muziki.
Pia siku hiyo kitatoka kitabu cha historia yake kichopewa jina la ‘A Very Good Bad Guy: The Story Of Innocent 2Face Idibia.’
Kitabu hicho kitajumuisha mahojiano ya kina na 2Face, maishari, mtazamo wa watu waliomsaidia katika maisha yake pamoja na mkusanyiko wa makala bora zilizowahi kuandikwa kumhusu tangu mwaka 2004.
Hicho kitakuwa ni kitabu cha kwanza cha aina yake katika kiwanda cha muziki wa Nigeria.

No comments

Powered by Blogger.