Image result for tigo banner

Diamond aitaja tarehe ambayo Tiffah ataoneshwa sura kwa mara ya kwanza

Hatimaye Diamond ameitaja tarehe ambayo sura ya binti yake Tiffah itaoneshwa hadharani kwa mara ya kwanza.
tiffah new
Tarehe 20 Septemba ndiyo siku ambayo Diamond na Zari wamepanga kuitambulisha sura ya mtoto wao Latiffah kwa ulimwengu, lakini kuna jambo kubwa ambalo litaambatana na utambulisho huo.
Licha ya kuwa Tiffah mwenye umri wa mwezi mmoja ni balozi wa maduka ya nguo ya Baby Shop, lakini video na picha za kwanza zitakazoonesha sura yake kwa mara ya kwanza zimedhaminiwa na makampuni mengine pia ambayo bado hajayataja.
Kupitia Instagram Diamond ameandika;
“Tareh 20|09|2015 kwa mara ya kwanza sura ya Binti yangu @princess_tiffah tutaiweka hadharani…je ungependa kujua ni Kampuni gani imedhamini Video na Picha yake ya kwanza????.. Mbali na kuwa balozi wa #BABYSHOP ya @Msasanicitymall & @Pugumall ungependa kujua amekuwa Balozi wa nini tena???.. uskae mbali na mimi… #TiffahsDay inakaribia..%) #ProudDad
(On the 20th of September 2015 my Daughter’s face @princess_tiffah will be Exclusively shown for the first time to the public… would you like to know which companies have sponsored her first video and photo??? Apart from being @MsasanicityMall and @PuguMall #BABYSHOP brand Ambassador would you like to know which companies have endorsed her??? Stay with me!!! #TIffahsDay Coming Soon..%)”
Toka hit maker huyo wa ‘Nana’, Diamond na mpenzi wake Zari wamlete duniani mtoto wao Tiffah mwezi mmoja uliopita, wamekuwa wakipost picha bila kumuonesha sura yake hali ambayo imeongeza shauku ya mashabiki kutaka kumuona

No comments

Powered by Blogger.