Navy Kenzo sasa waiongoza chati ya SoundCity Tv ya Nigeria
Wimbo wa Kundi la Navy Kenzo ‘Game’ unaendelea kufanya vizuri nchini Nigeria. Licha ya kuingia kwenye chati mbalimbali za Radio na Tv nchini humo, lakini pia unazidi kushika nafasi za juu.
Video yao ‘Game’ iliyofanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Justin Campos imekamata nafasi ya kwanza kwenye Top Ten East ya SoundCity Tv wiki hii. SoundCity kupitia akaunti yao ya Twitter na Instagram waliwapongeza Navy Kenzo.
Congrats @NavyKenzo! 'Game' ft. @VanessaMdee is #1 on this week's#SoundcityTopTenEast | http://t.co/IUv5nrubN2 pic.twitter.com/P2sY5FiDid
— Soundcity Africa (@SOUNDCITYtv) September 5, 2015
Post a Comment