Diamond ampiku Wizkid kwenye tuzo za ‘Uganda Entertainment Awards’
Diamond Platnumz ameibuka mshindi wa kipengele cha ‘Best African Act Of The Year’ Katika tuzo za Uganda Eentertainment Awards 2015 (UEA), zilizotolewa Ijumaa ya Septemba 5 jijini Kampala, Uganda.
Platnumz amewashinda mastaa wa Nigeria akiwemo Wizkid, Patoranking pamoja na Tiwa Savage ambao alikuwa akishindana nao kwenye kipengele hicho.
Kupitia mitandao ya kijamii Diamond amewashukuru mashabiki wake kwa kufanikisha ushindi huo kutokana na kura zao.
“My People!!! Jus Wanna thank you for your Vote and let you know that have won the BEST AFRICAN ACT OF THE YEAR on @uganda_entertainment_awards … S/O to my bro @tommyleeafrica for representing me and the whole @wcb_wasafi … Lastly wanna thank @uganda_entertainment_awards for recognize my Efforts…please keep VOTE for me on other Awards @neaawards @africanentertainmentawards @AfrimmaAwards #AfrimaAwards
(Ningependa kuwashkuru kwa kura mlizonipigia na kuwajuza kuwa kijana wenu nimefanikiwa kushinda tunzo ya Msanii Bora Africa katika tunzo za @uganda_entertainment_awards …nawashkuru na Daima nitaendelea kuwa Mchapa kazi na kuwa Balozi Mzuri wa Muziki wetu, Tafadhali tuendelee kupiga katika tunzo zilizo baki ili na sisi tuzidi kuuweka mziki wetu kwenye Ramani nzuri…. @neaawards @AfrmmaAwards
@africanentertainmentawards #AFRIMAAWARDS )”
@africanentertainmentawards #AFRIMAAWARDS )”
Post a Comment