Facebook sasa kuja na kitufe cha 'Dislike'
Facebook
ndio mtandao wa Kijamii ambao unatumiwa na watu wengi zaidi, Takwimu
zinaonesha Duniani kuna jumla ya watu kama Bilioni 7 hivi, alafu Ripoti
ya The Statistics Portal 2015 inaonesha watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wako Bilioni 1.96, na kati yao zaidi ya 70% ni watumiaji wa mtandao wa Facebook !!
Mark Zuckerberg katupasha kuhusu mipango mingine ya Facebook, sasahivi kama ukiandika post yoyote au ukiingia kwenye ukurasa wa mtu yoyote wa Facebook unakutana na alama tatu, alama ya ‘LIKE’, ‘COMMENT’ na alama ya ‘SHARE’… lakini CEO Zuckerberg anasema ni maombi ya muda mrefu watumiaji wa Facebook wanataka iwepo na alama ya DISLIKE, yani kama kitu hujakipenda unabonyeza tu hapo
Post a Comment