Image result for tigo banner

Nahreel azungumzia madai ya wimbo wa Game kufanana na wimbo wa Patoranking ‘Girlie O’

Mtayarishaji wa muziki na msanii, Nahreel amezungumzia madai ya kufanana kwa wimbo wa kundi lake Navy Kenzo, ‘Game’ pamoja wimbo wa ‘Girlie O’ wa msanii wa Nigeria, Patoranking.
game no5555
Nahreel ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM kuwa kabla wimbo huo haujatoka Patoranking aliusikia na kuusifia.
“Kiukweli cha kwanza kabla Game haijatoka Patoranking yeye mwenyewe aliisikia na anaipenda sana, ni wimbo anaoupenda,” alisema.
“Unajua watu wengi Tanzania wana mtindo huo wa kufananisha kitu kwa sababu pengine hawakubaliana na vitu. Kila vitu vizuri vinavyokuja hawakubaliani navyo, hivi vitu vinawezekana. Game imesifiwa na wasanii wakubwa kama Don Jazzy, 2face, P-Square, wame-comment kupitia Vanessa,” alisisitiza.
“Wenzetu wanaangalia muziki, hawaangalii sijui nani kafanya nini. Lakini Tanzania sisi inabidi tuache hiyo tabia na tusupport vizuri. Patoranking mwenyewe ingekuwa kashasema kitu kwasababu tupo naye karibu.”

No comments

Powered by Blogger.