Kisa cha Nahodha wa Negeria kujiondoa kikosi
Nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria na golikipa wa klabu ya Lille ya Ufaransa Vincent Enyeama, siku ya Septemba 2 ameingia katika headlines na shirikisho la mpira wa miguu Nigeria (NFF). Enyeama anaingia katika headlines baada ya kujitoa katika timu ya taifa kwa matatizo anayodai ni ya kifamilia.
Kwa mujibu wa mtandao wa ripples.com nahodha huyo wa timu Nigeria, alituma meseji kwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Sunday Oliseh na kueleza uamuzi wake kwa nini amejiengue katika timu yake ya taifa kwa sasa na hawezi kuwepo katika mechi zote muhimu.
Enyeama
anaeleza kuwa hawezi kuwepo, ana matatizo ya kifamilia ambayo
yanahitaji uangalizi wake hivyo hawezi kuwepo, taarifa hizi zinakuja
ikiwa ni siku chache zimebaki kabla ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, kuja Tanzania kucheza mechi na Taifa Stars Septemba 5 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Post a Comment